Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba achoma moto nyumba yake na mtoto ndani, adai kuna mwizi

Breaking: Moto Mkubwa Wazuka Tabora Mwanaume achoma moto nyumba yake na mtoto ndani, adai kulikuwa na mwizi

Tue, 10 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mjini Nanyuki wanamzuilia mwanamume mwenye umri wa miaka 48 ambaye aliwashangaza wakazi kwa kuchoma nyumba yake na kumwacha mtoto wa miaka 14 amefariki katika eneo la Kabiru, kaunti ya Laikipia.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Laikipia John Nyoike alisema kisa hicho bado kinachunguzwa ili kubaini kilichopelekea kitendo hicho kiovu.

"Mshukiwa mmoja aliyejulikana kwa jina la David Wang'ondu ambaye anaishi katika nyumba hiyo alikamatwa na alidaiwa kuchoma nyumba hiyo kwa sababu kulikuwa na mwizi ndani," alisema Nyoike.

Nyoike alisema waliarifiwa kuhusu uhalifu huo na chifu wa eneo la Majengo Duncan Wachira na walipozuru eneo la tukio na wakapata mwili wa mtoto huyo ndani ya nyumba hiyo. Mtoto huyo  alitambuliwa kama Christine Chelagat.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa chifu wa eneo la Majengo kuwa nyumba iliyo jirani na kanisa la KAG iliyo Kabiru inateketea kwa moto, polisi walitembelea eneo la tukio na kukuta moto umeshazimwa lakini ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na mwili wa marehemu mwenye umri wa miaka 14. mzee wa ujana,” alisema bosi wa polisi.

Waliozungumza na vyombo vya habari kwa sharti la kutotajwa majina yao kwa kuwa hawaruhusiwi kuzungumza walidai inawezeka mshukiwa alimnajisi mtoto huyo na kuchoma nyumba ili kuficha ushahidi.

Mwili huo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Nanyuki kusubiri uchunguzi wa maiti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live