Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu wa madrasa anayeshukiwa kuwabaka watoto akamatwa

Mwalimu Wa Madrasa Anayeshukiwa Kuwabaka Watoto Akamatwa Mwalimu wa madrasa anayeshukiwa kuwabaka watoto akamatwa

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: Voa

Mwalimu huyo anatuhumiwa kuwabaka wanafunzi 27 wa kike katika madrasa yake kwenye mji mtakatifu wa Touba uliopo katikati mwa Senegal, afisa wa polisi wa mji huo amesema.

Mwalimu wa madrasa nchini Senegal anayeshukiwa kuwabaka wanafunzi wake 27 wa kike alikamatwa Jumatatu baada ya wiki kadhaa za kukimbia chanzo cha polisi kimeliambia shirika la habari la AFP.

Mwalimu huyo anatuhumiwa kuwabaka wanafunzi katika madrasa yake katika mji mtakatifu wa Touba uliopo kati-kati mwa Senegal, afisa wa polisi wa mji huo amesema.

Mshukiwa huyo alitoweka baada ya tuhuma hizo kuibuka mapema mwaka huu kufuatia malalamiko kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa waathirika waliotoa vyeti vya matibabu, chanzo hicho kimeongeza. Alikamatwa siku ya Jumatatu baada ya kujisalimisha kwa polisi. Baada ya kuhojiwa, alikabidhiwa kwa vyombo vya usalama afisa huyo alisema.

Chanzo hicho kimesema mwalimu huyo anatuhumiwa kwa kuwabaka wanafunzi 27, lakini hakutoa maelezo sahihi kuhusu tarehe za madai ya uhalifu au umri wa walalamikaji.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa watu wanaodaiwa kuwa waathirika walikuwa watoto, ikiashiria kuwa walikuwa chini ya miaka 15 na kwamba shule au madrasa hiyo ya Korani imefungwa.

Chanzo: Voa