Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu wa Chuo atembezwa uchi kwa unyanyasaji wa Wanafunzi

Lectureeeee Mwalimu wa Chuo atembezwa uchi kwa unyanyasaji wa Wanafunzi

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhadhiri wa Chuo Kikuu kimoja kilichopo jimbo la Kogi nchini Nigeria, siku ya Ijumaa ya Mei 10, alijikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kuvuliwa nguo hadharani na kutembezwa akiwa na boxer pekee.

Chanzo kinasema wanafunzi chuoni hapo waliamua kumvua nguo mwalimu wao ili wamtie aibu baada ya kudaiwa kufanya unyanyasaji wa kingono kwa mwanafunzi mmoja wa kike wa chuo hicho.

Mhadhiri huyo alizua hasira kali miongoni mwa wanafunzi wa kike, waliokuwa wakisisitiza lazima ‘aaibishwe’ hadharani kwasababu wamechoshwa na tabia zake mbaya.

Hata hivyo baada ya muda mhadhiri huyo alikuja kuokolewa na walinzi wa chuo hicho na kutokomea kusikojulikana kwa aibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live