Pauline Mwalimu amesimuliA jinsi alivyopoteza alivyopoteza shilingi elfu mia moja na tano kwa walaghai, waliomlaghai kumtumia pesa kwa simu ili awape pesa taslimu.
Mwalimu, alipata kazi hii inayompa malipo ya shilingi elfu sita kwa mwezi ambayo anakiri kuwa inatimiza mahitaji yke na mwanaye.
Kwa bahati mbaya, Pauline ameanguka mikononi mwa kundi ambalo huwalenga wakala wa maduka ya M-pesa na kuwalaghai.
Akipiga kisengere nyuma, Pauline anakumbuka akifuatwa na mteja mmoja ambaye alimtambua kama Ben kutoka kaunti y kitui akiuliza begi lililoachwa nyuma. kabla ya kumkabili begi hilo, Ben aliitisha vocha ya simu ambayo Pauline alimtumia kutoka kwa simu ya M-pesa.
Pauline anasema kuwa;
"Mwanamke mmoja mgeni kabisa aliingia dukani akiwa amebeba beli la ununuzi siku iliyopita akasema alikua alikuwa ameelekezwa dukani na Ben na akaniomba nimshikie begi ili afanye shughuli fulani .'
Baadaye, mwanmke anayetambulika kama Faaith aliingia dukani na kuomba begi lililoachwa. Lakini kabla ya kumkabidhi begi hilo, anashauriwa kushiriki biashara ya kuuza uzi. Faith na mwenzake walimsawishi pauline kushiriki biashara hiyo wakidai kuwa ina faida kubwa.
Wawili hao wakimwibia Pauline siri kuwa, angepata faida ya hadi shilingi elfu 3,000 kwa uzi mmoja na kuanzia hapo hakujua kilihotokea, kwani anachokumbuka ni kuwa aliwakabidhi kima cha pesa.
"Kitu pekee ninanchokumbuka, ni kwamba niliwatumia walaghai pesa zote nilizokuwa nazo kwa simu. Niliingia katika misururu ya kukopa psa zaidi kutoka kwa marafiki na wafanyabiashara siokoni, ambazo kwa jumla niliwapa walaghai shilingi elfu 105,000."
Mwajiri wake na marafiki wake aliokopesha pesa, waliishia kumshuku kuwa alikua amepanga njama na walaghai hao.
Josph mwalimu, alipiga ripoti katika kituo cha Matuu lakini akabaini kuwa pilisi walichukua muda kuwakamata watapeli hao.
Jambo ambalo lilipelekea wao kuanza kuchanga pesa ili kurudisha zilizopotea ambapo walifanikiwa kukusanya shilingi elfu 31,000 pekee.
Mtaalamu wa usalama wa mtandao Allan Lwala alieleza kuwa , huenda Pauline alilemewa na dawa za kulvya wakati wa tukio. Alibaini kuwa, walaghai hao walitumia dawa ya scopolamine kweny uso wake au kupitia mguso wa kimwili.
Allan alitoa maelezo kuwa wakati mwingine dawa hizo zinaweza zikadhuru afya au kusababisha kifo, akisema kufikia sasa hakuna mbinu zilizobuniwa kukabili ujanja huo.
Haya yanajiri baada ya miezi michache iliyopita ambapo kisa sawia na hiki,kilichohusisha mwanasiasa mmoja wa Roots Party kiliripotiwa akilaghaiwa zaidi ya shilingi elfu 100,00.