Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu aliyemcharaza mwanafunzi wa miaka 9 viboko 107 afikishwa kortini

Sdrg Mbaroni Mwalimu aliyemcharaza mwanafunzi wa miaka 9 viboko 107 afikishwa kortini

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jackson M. Marucha, Mwalimu kutoka Kaunti ya Nyamira Kenya, anatuhumiwa kumpa adhabu hiyo Mwanafunzi wa Darasa la 4 mwenye miaka 9 baada ya kuripoti kuibiwa nguo zake za Shule.

Mwalimu alijaribu kuficha kitendo hicho kwa kumfungia Mwanafunzi Bwenini na kumnyima matibabu baada ya kugundua ana majeraha makubwa mwilini mwake.

Hata hivyo, ndugu wa Mwanafunzi aliyepata taarifa, alizuiwa na Uongozi wa Shule kumuona kwa kuhofia kugundulika hali aliyonayo. Mwalimu huyo amepandishwa Kizimbani ikiwa ni miezi 2 tangu kuripotiwa tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live