Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu ajinyonga kisa 'ex' atoa maagizo azikwe Valentine Day

Kifo Mautii Mwalimu ajinyonga kisa 'ex' atoa maagizo azikwe Valentine Day

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu wa shule ya sekondari iliyopo Kijiji cha Nthangathiri, Kaunti ya Embu nchini Kenya, amejiua kwa kujitundika kitanzi ndani ya nyumba yake baada ya kukataliwa na mpenzi wake zamani.

Polisi nchini Kenya imeeleza kwamba marehemu Dennis Mwaniki Njeru (32) alikutwa amefariki dunia chumbani kwake, huku kukiwa na ujumbe wa barua pembeni yake akiacha maagizo azikwe Siku ya Wapendanao.

Tovuti ya Taifa Leo imeeleza kwamba kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi, Njeru alikuwa anavuja povu puani, pia kemikali inayodhaniwa kuwa ni dawa ya kuua wadudu ilikutwa ndani ya chumba hicho.

Imeelezwa ujumbe aliouacha Njeru, ulisomeka kwamba alifanya uamuzi wa kujitoa uhai kutokana na kukataliwa na mpenzi wake.

“Naweza nikaonekana mjinga lakini nimefungua moyo wangu kuhusu kinachoniumiza …acha tukutane mbinguni. Nimemsihi mpenzi wangu lakini yote nimeambulia patupu. Nawapenda nyote,” alisema kupitia barua hiyo.

Hata hivyo, imeelezwa mtu huyo ameacha maagizo pia kuhusu jinsi anavyotaka kuzikwa.

Ameagiza ofisa mkuu katika Bunge la Kaunti pamoja na diwani wa eneo hilo kuongoza mipango ya mazishi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live