Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaua watu 50 Rwanda

Mvua Imesababisha Vifo Vya Watu 4 Huko DRC Mvua yaua watu 50 Rwanda

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua kubwa iliyonyesha nchini Rwanda inaripotiwa kusababisha vifo vya watu wasiopungua 50.

Waziri wa Masuala ya Dharura nchini Rwanda Albert Murasira amesema, athari zilizotokana na mvua kubwa yakiwemo maporomoko ya udongo na radi, zimesababisha vifo vya watu 50 na wengine 79 kujeruhiwa nchini humo katika miezi miwili iliyopita.

Murasira amesema kuuwa, watu 12 wamefariki kwa kupigwa na radi huku wengine wakifariki kwa kuangukiwa na nyumba zao mbovu.

Waziri huyo aidha amesema, serikali imewahamisha wakazi karibu elfu 5 kutoka maeneo yenye hatari kubwa hadi maeneo salama kote nchini.

Maafa hayo pia yameharibu miundombinu, ikiwemo nyumba, madaraja, majengo ya shule, mitandao ya barabara pamoja na mashamba.

Wakati huo huo, Rwanda, imetangaza kwamba kutokana na mvua kubwa iliyotabiriwa katika wiki ya kwanza ya Mei, baadhi ya mito inaweza kuvunja kingo zake na kusababisha mafuriko katika jamii.

Tahadhari hiyo imetolewa na Bodi ya Rasilimali za Maji ya Rwanda (RWB), na kusisitiza kuwa, mito inayoweza kusababisha mafuriko ni pamoja na Mto Sebeya, Karambo, Nyabahanga, Kabirizi, Nyabarongo, Mwogo, Mukungwa, Rubyiro, Cyagara, pamoja na mito ya Ukanda wa Virunga.

Mvua kubwa za msimu huu tayari zimesababisha maafa nchini Rwanda na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki hususan Kenya na Tanzania. Zaidi ya watu mia tatu wameripotiwa kufarikki dunia katika nchi hizo mbili kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Mvua kubwa iliyosababishwa na El NiƱo na mafuriko vinaendelea kuathiri sehemu za ukanda wa Afrika Mashariki, zikiwemo Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini na Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live