Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yasababisha maafa Kenya

Wed, 22 Apr 2020 Chanzo: --

KARIBU watu 12 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Kenya.

Mshirikishi wa eneo la Bonde la Ufa, George Natembeya alisema watu sita wakiwemo maofisa wawili wa polisi, wamefariki katika maporomoko ya udongo yaliyotokea kwenye mpaka wa kaunti za Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa Jumamosi hadi Jumapili.

Kadhalika watu wengine sita wameripotiwa kufariki dunia katika eneo la Chesogon kauti ya Pokot Magharibi kutokana na mafuriko, mbali na mamia ya familia kuachwa bila makazi.

Habari zaidi zinasema kuwa, kuna watu kadhaa ambao hawajulikani walipo kutokana na mafuriko hayo, huku timu za uokoaji zikiendelea kuwatafuta kando ya Mto Chesogon.

Aidha wakazi wa eneo hilo wametakiwa kuhamia nyanda za juu na kwenye maeneo salama ili kuepusha maafa zaidi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo.

Chanzo: --