Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua imesababisha vifo vya watu 4 huko DRC

Mvua Imesababisha Vifo Vya Watu 4 Huko DRC Mvua imesababisha vifo vya watu 4 huko DRC

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: Voa

Watu watano waliokolewa na wengine 20 walisombwa na maji. Juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa wengine zinaendelea katika eneo.

Mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya ardhi mashariki mwa Congo usiku wa kuamkia Jumatatu na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wanne na kuwaacha wengine 20 wakiwa hawajulikani waliko, afisa mmoja wa eneo hilo amesema.

Maporomoko hayo yalitokea Jumapili jioni karibu na mji wa Kamituga katika mkoa wa Kivu Kusini kulingana na Naibu Meya Alexandre Ngandu Kamundala. Kiasi cha watu 25 wengi wao wakiwa wachimba migodi walipata hifadhi kutokana na mvua zilizonyesha kwenye mabanda wakati maporomoko ya ardhi yalipochukua makazi yao na kuyapeleka katika mto uliofurika, Kamundala alisema.

Watu watano waliokolewa kwa urahisi na wengine 20 walisombwa na maji. Miili minne ilipatikana ikiwa imekufa, alisema Kamundala. Juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa zinaendelea ili kuwapata wale ambao bado hawajulikani waliko. Mwaka 2020 watu wasiopungua 50 katika mji huo huo wa Kamituga walifariki dunia katika maporomoko ya ardhi yaliyopiga eneo la mgodi wa dhahabu katika eneo hilo.

Ajali zinazopelekea vifo ni za kawaida katika migodi mingi ambayo haijadhibitiwa nchini Kongo huku idadi kubwa ya vifo haviripotiwi kutokana na maeneo yao madogo kuwepo katika milima na misitu.

Chanzo: Voa