Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvinyo waua watano Kenya

Pombepicha Mvinyo waua watano Kenya

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Inasemekana kwamba sita hao walibugia pombe hiyo katika eneo la JC lililoko Kabatini kaunti ndogo ya Nakuru KaskaziniMiili minne ilipatikana katika maeneo mbali mbali kiwanjani na mtu wa tano naye aliaga dunia akipokea mtibabu katika hospitali ya BahatiSampuli zimechukuliwa kutoka kwa miili ya waathiriwa kufanyiwa uchunguzi kamiliWatu watano wameaga dunia baada ya kushukiwa kunywa pombe aina ya chang’aa yenye sumu huku mwengine naye akilazwa katika hospitali ya Bahati akiwa hali mahututi.

Inasemekana kwamba sita hao walibugia pombe hiyo katika eneo la JC lililoko Kabatini kaunti ndogo ya Nakuru Kaskazini mnamo Jumatatu, Agosti 7.

Wenyeji walisema kwamba mtu wa sita ambaye yuko hali mahututi alianza kulalamikia maumivu ya tumbo kabla ya kuzirai kulingana na ripoti ya Citizen TV.

Kamanda wa Nakuru Beatrice Kiraguri mnamo Jumanne, Agosti 8 alisema kwamba haikubainika ni nini haswa wanne hao walikuwa wamekula kwani miili yao ilipatikana sehemu tofauti tofauti.

Miili minne ilipatikana katika maeneo mbali mbali kiwanjani na mtu wa tano naye aliaga dunia akipokea mtibabu katika hospitali ya Bahati.

Read also

Hofu Yatanda Baada ya Wasichana 9 Kutoweka Shuleni Katika Hali ya Kutatanisha

Kiraguri alisema ilikuwa vigumu kubaini walichokila waathiriwa kwani hamna mtu yeyoye ambaye alitaka kutoa taarifa kwa polisi.

“Hata aliyeponea ameshindwa kusema walichokila. Ni mzee wa Kijiji ambaye alitupa taarifa na kusema kwamba wanashukiwa walikunywa pombe aina ya chang’aa ambayo ilikuwa imetiwa sumu,” alidokeza.

Alifafanua kwamba huenda walikula chakula au kunywa kitu kilichowadhuru.

Kiraguri alisema kwamba sampuli zimechukuliwa kutoka kwa waathiriwa na mwenzao aliyeponea ili kufanya uchunguzi na kubaini kilichosababisha vifo vyao.

“Inashukiwa kwamba chang’aa waliyoinywa ilitiwa sumu na muuzaji wa karibu ambaye alikuwa akizozana na mwenzake akidai aliiba bidhaa zake, lakini kwa sasa hatuwezi kudhibitisha hilo hadi pale ambapo watu watajitokeza na kutoa ushahidi,” alisema.

Miili yao imepelekwa hatika makafani hospitali ya Bahati.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke