Msajili wa Vyama vya Kisiasa Ann Nderitu ametoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na hatma ya muungano wa National Super Alliance (NASA).
Aliwatumia Raila, Mudavadi, Kalonzo, Wetangula na Isaac Ruto baura ya kubalibainisha kuwa maazimio hayo yalitekelezwa kwa utaratibu uliostahiliMnamo Agosti 3, 2021 viongozi wa chama cha Wiper, ANC, na Ford-Kenya walitangaza azimio lao la kuondoka katika NASA, uamuzi ambao uliisukuma ODM pia kung'atuka.
Nderitu alithibitisha kuvunjwa kwa muungano huo baada vyama vya Wiper, ANC, Ford Kenya, na Chama Cha Mashinani, kumuandikia barua ya kufanya uamuzi wa kuhama NASA.
Mnamo Ijumaa, Agosti 27, Nderitu alithibitisha kuvunjwa kwa muungano huo baada ya Wiper Democratic Movement, Amani National Congress (ANC), Ford Kenya, na Chama Cha Mashinani, kumuandikia barua ya kufanya uamuzi wa kuhama NASA.
Kupitia barua aliyowatumia kinara wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), Raila Odinga, Musialia Mudavadi wa ANC, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Moses Wetangula wa FORD-Kenya, na Isaac Ruto wa Chama Cha Mashinani, alibainisha kuwa maazimio hayo yalitekelezwa kwa utaratibu uliostahili.
Read also
DP Ruto Ajitenga na UDA, Asisitiza Yeye ni Naibu Kiongozi wa Jubilee
"Afisi hii, kulingana na Kanuni ya 22 (2) ya Usajili wa Vyama vya Siasa 2019, itachapisha katika magazeti mawili kuvunjwa kwa muungano huu," Nderitu alisema.
Mnamo Agosti 3, 2021 viongozi wa chama cha Wiper, ANC, na Ford-Kenya walitangaza azimio lao la kuondoka katika NASA, uamuzi ambao uliisukuma ODM pia kung'atuka katika muungano huo.
Uamuzi wa kujiondoka katika NASA ulijiri baada ya Raila kukubali kugawa pesa akifichua kwamba ODM itagawa KSh 153 milioni biana ya wanachama wake wakuu na kuhifadhi Ksh334.6 milioni.
Chama cha Wiper kilipokea Ksh70.4 milioni na ANC Ksh 43.8 milioni.
Hatua hiyo ilipelekea kwa vyama hivyo kutafuta ushirikiano kwingine kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2022.
Kufikia sasa, ODM imo mbioni kuunda muungano na chama tawala cha Jubilee wakati ANC, WIPER, Ford-Kenya na KANU waliafikiana kuingia katika muungano wa One Kenya Alliance (OKA).
Viongozi hao wamekuwa wakikutana na Rais Uhuru Kenyatta katika kile ambacho kimeonekana kama njia ya kuimarisha vyama vyote vya upinzani.
Read also
Uhuru Aelekea Zambia Kujiunga na Raila Katika Hafla ya Kumuapisha Rais wa Zambia Hakainde Hichilema
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.