Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muungano wa Handisheki: Jubilee na ODM Wakutana Kuweka Mikakati

30cc654220565809 Muungano wa Handisheki: Jubilee na ODM Wakutana Kuweka Mikakati

Fri, 18 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wandani wa Rais na wale wa Raila walikutana jijini kuanza mazungumzo ya kuwa na mgombea mmojaKikao hicho kilijiri siku chache baada ya ripoti kuwa Rais amewataka NASA kuungana ili amuunge mgombea wao 2022Ni ripoti ambazo zimewasha moto kwenye kambi za kisiasa haswa upande wa DP RutoMbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed ameashiria kuna mpango wa kuunda muungano kati ya Jubilee na ODM.

Akiongea na runinga ya KTN Juni 17, mbunge huyo alisema kuna 'mambo makubwa' ambayo yanajiri.

Junet ni mmoja wa wandani wa Raila Odinga na anapoketi sauti ya Raila huskika kwani huonekana kama mwakilishi wake.

Alisema walikuwa na kikao na wenzao kutoka Jubilee ili kujadili safari ya urafiki wao tangu Uhuru na Raila waingie kwenye handisheki.

"Tulikutana na uongozi wa Jubilee kwa chakula cha mchana ili kujadili vile tumekuwa tukishirikiana. Tulijadili pia masuala mazito. Mambo makubwa yanajiri na tunataka kuhakikisha urafiki wetu ni bora zaidi," alisema mbunge huyo

Kulingana na gazeti la Daily Nation, kambi za Raila na Uhuru zilifanya kikao kwenye mkahawa jijini ambapo walianza kujadili uwezekano wa kuwa na mgombea mmoja.

Kulingana na gazeti hilo, mbinu ni kujaribu kuwa na mgombea ambaye anaweza kukabiliana na DP Ruto kwenye uchaguzi wa kuingia Ikulu 2022.



Kwenye kikao hicho, upande wa Jubilee uliwakilishwa na katibu Raphael Tuju na naibu mwenyekiti David Murathe ambaye ni mwandani wa Rais Kenyatta wa karibu.

Kikosi cha ODM nacho kiliwakilishwa na katibu wao Edwin Sifuna na mbunge huyo wa Suna Mashariki.

Kikao chao kinajiri siku chache tu baada ya gazeti la Star humu nchini kuripoti kuwa Rais amekwisha fanya uamuzi wa kuunga mkono mgombea wa muungano wa NASA.

Ni taarifa ambazo zilimfanya Naibu Rais William Ruto kukosa usingizi akilalamika kusalitiwa baada ya kusimama na Uhuru kwa vipindi viwili.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke