Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muswada wa fedha 2024: Wabunge walengwa na waandamanaji

Muswada Wa Fedha 2024: Wabunge Walengwa Na Waandamanaji.png Muswada wa fedha 2024: Wabunge walengwa na waandamanaji

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Waandamanaji wanaopinga Muswada tata wa Fedha wa 2024 walivamia majengo na biashara zinazoaminika kumilikiwa na baadhi ya washirika wa Rais Ruto, haswa wale waliounga mkono muswada huo.

Wabunge wa Bunge la Taifa na Mabunge ya Kaunti walikuwa miongoni mwa waliolengwa.

Mjini Nyeri, waandamanaji walipora na kuchoma moto duka kuu la Chieni. Kulingana na ripoti, biashara hiyo ni ya Mbunge wa Kieni Njoroge Wainaina.

Kanda za video zilizosambazwa mitandaoni zinaonyesha majengo ya duka hilo kubwa yakiwaka moto wakati wa maandamano ya Jumanne.

Waandamanaji hao pia walivamia na kupora klabu ya usiku inahusishwa na mbunge Oscar Sudi, mshirika wa karibu wa rais, na kuharibu mali ya thamani isiyojulikana.

Katika kaunti ya Embu, waandamanaji pia walivamia na kuharibu afisi za bunge la kaunti, huku video zilizosambazwa mtandaoni zikionyesha afisi za bunge hilo zikiwaka moto.

Katika tukio lingine sawia na hilo, waandamanaji pia walichoma moto, afisi ya mbunge wa Igembe Kusini Paul Mwirigi.

Mbunge huyo alikuwa miongoni mwa wabunge waliopigia kura Muswada wa Fedha.

Na huko Machakos, vijana waliokuwa wakiandamana walivamia afisi za usalama za bunge la kaunti ya Machakos, na kuziharibu kabla ya kuziteketeza.

Chanzo: Bbc