Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonye aitosa FKF

F4489b5a94acc0f47278ecc4c0e96442 Musonye aitosa FKF

Tue, 15 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu wa zamani wa Baraza la Vyama vya Soka vya Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholas Musonye (pichani), ni miongoni mwa ambao hawajarejesha fomu katika Bodi ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF).

Mtu mwingine maarufu aliyeshindwa kurejesha fomu hiyo ni aliyekuwa Rais wa FKF, Sam Nyamweya. Kwa mujibu wa taarifa ya bodi hiyo, jana ilitarajia kufanya mawasiliano na wagombea kwa njia ya mtandao ili kuwapa maelekezo ya nini cha kufanya, pamoja na kuwa na kipindi cha maswali na majibu.

Maofisa watakaosimamia uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 17, watapewa semina itakayofanyika Septemba 17. Kamati ya Uchaguzi Mkuu wa FKF imetoa orodha ya mwisho ya majina matano ya watakaowania kiti hicho.

Mgombea, Nick Mwendwa, atakuwa na mgombea mwenza, Dori Petra. Wengine ni mwandishi wa habari za michezo, Boniface Osano na mgombea mwenza wake ni Innocent Mutiso, ambaye ni mwanasoka wa zamani.

Wagombea wengine ni mwenyekiti wa zamani wa AFC Leopards, Daniel Mule na mgombea mwenza, Peter Lichungu, Herbert Mwachiro, Harold Ndege na Lordvick Aduda atakayekuwa na Athanas Obala.

Wagombea waliofanikiwa walirejesha fomu kwa Bodi ya Uchaguzi iliyopo Kandanda House, Nairobi.

Awali, uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Septemba 19, lakini Mahakama ya Michezo nchini humo (SDT) iliuahirisha kwa madai kuwa kanuni na sheria zilipuuzwa.

Chanzo: habarileo.co.tz