Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni awakosea vikali Marekani kufuta mkataba

Museveni Kujadili Na Wabunge Muswada Dhidi Ya Mapenzi Jinsia Moja Museveni awakosea vikali Marekani kufuta mkataba

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameikosoa vikali Marekani kufuatia uamuzi wa hivi majuzi wa nchi hiyo wa kuiondoa Uganda kwenye mkataba mkubwa wa kibiashara na kutoa ushauri kwa wafanyabiashara wasiwekeze katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kufuatia kupitishwa kwa sheria kali ya kupiga marufuku uhusiano watu wa jinsia moja nchini Uganda, Marekani imedai kuwa eti sheria hiyo inakiuka haki za binadamu na hivyo imetangaza vikwazo dhidi ya nchi hiyo ambayo imesisitiza kuwa kamwe haitaruhusu uovu huo katika mipaka yake.

Wiki iliyopita, Marekani ilitangaza kuiondoa Uganda, pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gabon, na Niger, kutoka kwa Sheria yake ya Ukuaji na Fursa Afrika (AGOA). Mkataba wa AGOA unawezesha bidhaa za Afrika kuingia Marekani bila ushuru.

Rais Museveni amewahakikishia watu wa Uganda kwamba nchi inaweza kusonga mbele bila kuungwa mkono na ulimwengu wa Magharibi.

Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Museveni amewaambia watu wa Uganda hivi: "Nawashauri kuwa musiwe na wasiwasi kupita kiasi kuhusu hatua za hivi majuzi zilizochukuliwa na serikali ya Marekani ya kuzuia kampuni zao kuwekeza nchini Uganda na kuiondoa Uganda kwenye orodha ya AGOA."

Rais Museveni aliongeza kwamba: "Baadhi ya nchi katika ulimwengu wa Magharibi zinajikuza kupita kiasi na kuwadharau wapigania uhuru wa Afrika."

Aidha Rais wa Uganda amesema, ni dhana potofu kwa baadhi ya nchi za kigeni kudhani kuwa Afrika haiwezi kuendelea bila msaada wao.

Kampala mji mkuu wa Uganda "Kwa hakika, kwa upande wa Uganda, tuna uwezo wa kufikia malengo yetu ya ustawi na maendeleo, hata kama baadhi nchi hazituungi mkono," alisema.

Uganda imekuwa ikivutana na nchi za Magharibi tangu ipasishe sheria hiyo kali ya kukabiliana na vitendo viovu vya maingiliano haramu ya watu wa jinsia moja.

Mwezi Agosti mwaka huu pia, Benki ya Dunia ambayo ina makao yake mjini Washington, Marekani, ilionesha wazi jinsi ilivyo kibaraka wa madola ya Magharibi kwa kujiingiza katika masuala yasiyoihusu, kwa kusitisha mikopo mipya kwa Uganda kutokana na nchi hiyo ya Afrika Mashariki kupasisha sheria ya kupinga vitendo vichafu vya ubaradhuli.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni hivi karibuni pia alikataa wito wa nchi za Magharibi wa kufuta sheria hiyo dhidi ya vitendo viovu vya maingiliano haramu ya watu wa jinsia moja iliyopasishwa na Bunge la nchi hiyo na kuidhinishwa na yeye mwenyewe mwezi Mei mwaka huu.

Alisema, "Utiaji saini wa muswada wa kupinga ndoa za watu wenye jinsia moja umekamilika, hakuna mtu atakabadilisha hatua yetu. Tunapaswa kuwa tayari kwa mapambano."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live