Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni ataja sababu bomba la mafuta kupita Tanzania

455906473d48058f8ff84ca630326102 Museveni ataja sababu bomba la mafuta kupita Tanzania

Sun, 11 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ametaja sababu za Uganda kupitisha Bomba la Mafuta Tanzania ni kutokana na upekee wa historia wa nchi hizo mbili.

Museveni alisema kulikuwa na majadiliano bomba lipite Mombasa Kenya au Tanga Tanzania, lakini wakaamua kupitisha bomba hilo Tanzania kutokana na upekee wa historia kwa kuikomboa Uganda kutoka kwenye mikono ya Idd Amin Dada.

“Nchi ya Kenya ni kaka zetu kama walivyo Tanzania, lakini Tanzania ina upekee wake, mwaka 1978 /79 Mwalimu Nyerere anamchango mkubwa Uganda, alituondolea Idd Amin na Uganda ikapata Uhuru wake, pia ana mchango mkubwa kwenye ukombozi wa nchi za Afrika ikiwemo Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini,” alisema Museveni.

Alisema pia mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa Uganda, Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika nzima, na kwamba pamoja na faida zilizoainishwa kwa bomba hilo pia ni uwepo wa amani, uzoefu wa Tanzania katika uendeshaji wa miradi ya mabomba ya mafuta na gesi, jiografia nzuri ya usafirishaji mafuta, na viwango nafuu vya tozo

Chanzo: www.habarileo.co.tz