Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni apuuzia kuondolewa kwa Uganda mkataba wa kibiashara na Marekani

Museveni Apuuzilia Mbali Kuondolewa Kwa Uganda Kutoka Agoa Museveni apuuzia kuondolewa kwa Uganda mkataba wa kibiashara na Marekani

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa majaribio ya nje ya kuishawishi nchi hiyo ni ya bure, zaidi ya wiki moja baada ya nchi yake kufukuzwa kutoka kwa mpango maalum wa kibiashara wa Marekani na Afrika.

Marekani ilitishia kwa mara ya kwanza kuiwekea vikwazo Uganda na kuifukuza kutoka kwa Mkataba wa Biashara wa Ukuaji na Fursa Afrika (Agoa) mwezi Mei, baada ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kupitisha sheria yenye utata dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Sheria hiyo inaweka adhabu ya kifo kwa baadhi ya vitendo via wapenzi wa jinsia moja.

"Kwa sasa, wale wanaotuwekea shinikizo, wanapoteza muda wao. Na hatupaswi kuwa na wasiwasi kuhusu hilo," Rais Museveni alisema katika hotuba yake ya kitaifa siku ya Jumanne, akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kangazo hilo la Marekani.

"Tunachopaswa kuzingatia ni kupambana na ufisadi miongoni mwetu. Haya ndiyo matatizo halisi. Si shinikizo la nje, kwa sababu hilo halina maana," aliongeza.

Bw Museveni pia alisema kuwa Uganda itafanya biashara na washirika wa kimataifa ambao "wanaiheshimu".

Chanzo: Bbc