Uganda imekejeli onyo la Marekani kuhusu hatari ya kufanya biashara katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, na kulitaja kuwa "la kuchekesha".
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilichapisha ushauri siku ya Jumatatu ikiwataka wawekezaji watarajiwa kuwa makini na "rushwa iliyoenea" na ukosefu wa heshima kwa haki za binadamu nchini Uganda.
Baada ya hapo Ilifuatia onyo jipya la kusafiri lililotolewa na Washington mapema mwaka huu baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kutia saini kuwa sheria mswada mkali wa kupinga ushoga.
"Biashara, mashirika, na watu binafsi wanapaswa kufahamu hatari zinazoweza kutokea za kifedha na sifa zinazotokana na ufisadi uliokithiri," ushauri huo ulisema.
Lakini Pia ilionya kuhusu "vurugu dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu, wanahabari, wafanyakazi wa afya, wanachama wa makundi madogo, watu wa LGBTQI+, na wapinzani wa kisiasa".
Kufutia Kupitisha kwa Uganda Sheria ya Kupinga Ushoga mwezi Mei kulizua hasira miongoni mwa makundi ya haki za binadamu, wanaharakati wa LGBTQ, Umoja wa Mataifa na mataifa yenye nguvu za Magharibi huku Rais wa Marekani Joe Biden alitoa wito wa kufutwa mara moja kwa hatua hizo na kutishia kupunguza misaada na uwekezaji nchini Uganda, huku Benki ya Dunia ikitangaza kuwa inasitisha mikopo mipya kwa nchi hiyo.
Uganda inashika nafasi ya 142 kati ya nchi 180 kwenye Kielezo cha Mitizamo ya Ufisadi cha Transparency International.
Waziri mdogo wa habari wa Uganda, Godfrey Kabbyanga, aliwataka wawekezaji wa Marekani kupuuza onyo la Wizara ya Mambo ya Nje.