Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni apewa dozi ya pili ya COVID-19

8ab34761cc3dd5fec4efe46eab1a518d.jpeg Museveni apewa dozi ya pili ya COVID-19

Sat, 5 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, amepata chanjo ya pili na ya mwisho dhidi ya virusi vya corona (COVID-19).

Taarifa ya Ikulu ya Uganda iliyotolewa jana ilisema Rais Museveni alipewa dozi ya pili ya chanjo na ya mwisho dhidi ya COVID-19, na kuwataka wananchi wa nchi hiyo kufuata taratibu za kujikinga ugonjwa huo sambamba na kupata chanjo.

Rais Museveni alisema chanjo ya corona itaanza kutolewa kwa makundi ya watu walio hatarini kukumbwa na ugonjwa huo wakiwemo wahudumu wa afya, walimu, walinzi wa usalama, na kwamba lengo la nchi hiyo ni kuwachanja watu milioni nne.

Rais Museveni amewahakikishia wananchi kuwa chanjo ni salama na ina ufanisi hivyo wasiogope kuchanjwa, bali wajitokeze kwa wingi kupokea chanjo.

Wakati hayo yakijiri nchini Uganda, Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zimezitaka nchi zinazotarajiwa kupata dozi za ziada za chanjo dhidi ya corona, katika miezi kadhaa ijayo, kusambaza dozi hizo haraka iwezekanavyo kwa nchi zinazoendelea.

Aidha, taasisi hizo zimezihimiza jamii za kimataifa kutoa msaada wa fedha Dola za Marekani bilioni 50, ili kutimiza upatikanaji sawa wa chanjo, na kusaidia kupambana na kuenea kwa virusi vya corona duniani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz