Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni aongeza siku 21 za kukaa ndani Uganda

102421 Uganda+pic Museveni aongeza siku 21 za kukaa ndani Uganda

Tue, 14 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala. Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameongeza siku 21 za wananchi kukaa ndani kuanzia kesho Aprili 15 hadi Mei 5, 2020 baada ya siku 14 za kwanza kumalizika leo lengo likiwa ni kujikinga na maambuziki ya corona. Ameongeza kuwa wameongeza siku 21 baada ya kuwepo kwa mafanikio kwa muda wiki tatu tangu kuanza kutangazwa uamuzi hayo. Museveni amesema suala la usafiri wa umma litajadiliwa na kupendekeza usafiri wa baiskeli kwa sababu unabeba mtu mmoja na ni wa afya. Amesema kabla ya ugonjwa huo kuingia asilimia 40 ya watu walikuwa wanakufa hospitali kwasababu ya kula sana na kutofanya mazoezi kwa hiyo baiskeli zitasaidia.

Chanzo: mwananchi.co.tz