Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni aongeza jina kuelekea uchaguzi mkuu

4056f1ec29177fa8efac83fea3be7c46 Museveni aongeza jina kuelekea uchaguzi mkuu

Tue, 13 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Rais Yoweri Museveni ameapa tamko kisheria la kurekebisha majina yake ili yaandikwe kwa mpangilio mzuri kulingana na sheria ya usajili wa majina na kuongeza katikati jina la la Tibuhaburwa hivyo majina yake kutambulika kama Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni.

Sheria mpya ya Usajili wa Watu imesababisha wanasiasa wengi na viongozi wa umma kufanya marekebisho katika mpangilio wa majina yao ili kuepuka hatari ya kupoteza uteuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

Mnamo Oktoba 6, mwaka huu , Museveni aliapa katika hati ambayo gazeti la Daily Monitor imeliona, ambapo anaelezea kulazimika kuweka majina yake katika mpangilio mzuri kutokana na kuandikwa bila mpangilio.

Katika hati ya kiapo, Rais Museveni alisema alizaliwa Septemba 1944 na kutambulika kwa jina Yoweri Tibuhaburwa Kaguta,inaelezwa kuwa vyeti vyake vya masomo jina lake Yoweri Tibuhaburwa Museveni.

"tangu nilipomaliza masomo yangu, majina Yoweri Museveni, Yoweri Tibuhaburwa Museveni, Yoweri Kaguta Museveni na Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni yametumika kwa kubadilishana ," anasema Museveni katika hati ya kiapo.

Inaelezwa kuwa katika uchaguzi mkuu mwakani akipeperusha bendera ya chama tawala cha National Resistance Movement anasema kuanzia Oktoba 6 na kuendelea, kisheria atatambulika kwa jina sahihi la Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni.

"Kwa madhumuni ya kudhibitisha mpangilio mzuri wa jina langu kamili, natangaza kwamba kuanzia sasa katika rekodi zote, katika hafla zote zinazohitaji utumiaji kamili jina, saini jina la Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni badala ya majina niliyobadilisha. ”

Inaelezwa kiapo hicho kilifanywa na kampuni ya sheria ya K&K law firm na mmoja wa mameneja Kiryowa Kiwanuka,alithibitisha rais kula kiapo hicho.

Chanzo: habarileo.co.tz