Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni amtuhumu Bobi Wine kuiba kura

Museveni Bobi Wine 660x400.jpeg Museveni amtuhumu Bobi Wine kuiba kura

Tue, 16 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Kwa mara ya kwanza Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekituhumu chama cha siasa cha NUP kwa kuhusika na vitendo vya udaganyifu wa wizi wa kura katika zoezi la uchauzi mkuu uliofanyika tarehe 14 January 2021.

Museveni amesema madai ya Kyagulanyi yaani Bobi Wine kwamba ushindi wake katika uchaguzi mkuu ulichukuliwa na rais Museveni na kumutaka kurudisha maamuzi ya wananchi.

Katika hotuba yake usiku wa kuamukia leo rais Museveni amedai kwamba chama cha NUP kilifanya udaganyifu mkubwa katika zoezi la uchaguzi mkuu wa rais na wabunge ndiyo sababu walipata kura hizo hasa katika mkoa wa kati na baadhi ya sehemu za mkoa wa Busoga na kumuonya Kiongozi wa chama cha NUP mipango yake anayopanga kufanya ya maandamano:

“Ni upande wa upinzani hususani kundi la Kyagulanyi ambao walifanya udaganyifu mkubwa kila mtu nchini Uganda anafahamu nani aliyeiba ni kundi la Kyagulanyi, hizo kura wanazodai zaidi ya milioni tatu hazipo, kulikuwa na vitisho vilivyofanywa na wafasi wa NUP” Museveni

“Na sasa wapinzani wanapanga kuzuia kuapishwa rais hawawezi yoyote anayepanga jeshi litawakamata,” Museveni MAMA SAMIA AFUNGUKA “MSISIKILIZE MANENO YA KUTOKA NJE”

Chanzo: millardayo.com