Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni alaumu mashambulizi ya ADF kutokana na dosari za kijasusi

Museveni Alaumu Mashambulizi Ya ADF Kutokana Na Dosari Za Kijasusi Museveni alaumu mashambulizi ya ADF kutokana na dosari za kijasusi

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Rais Yoweri Msevei wa Uganda amesema kwamba kikundi cha wapiganaji cha ADF kimevunjika katika makundi madogo madogo ambayo imekuwa vigumu kuyatambua huku akitoa wito wa kuimarishwa kwa ujasusi.

Katika hotuba ya kitaifa kuhusu ugaidi na uhalifu , rais Museveni alitaja kuwatafuta wapiganaji hao ni sawa na kutafuta sindano katika rundo la nyasi , lakini akasisitiza kwamba kazi ya kuwasaka watu binafsi wa kundi hilo inawezekana iwapo kuna ujasusi wa hali ya juu na ushirikiano kati ya vitengo vya usalama na raia kulingana na mtandao wa the Monitor Uganda..

‘’Kwasasa hawawezi tena kufanya operesheni zao kiukubwaama katika makundi madogo. Sasa njia ya pekee wanavyoweza kufanya operesheni zao ni kibinfasi. Na kwanini hawawezei kufanya opereshei zao kwa makundi ni kwamba wakifanya hivyo watapatwa na maafa. Kwasababu tunaweza kuwaona na kuwakabili. Tuna uwezo wa kuwakabili’’, alisema.

Hotuba hiyo inajiri takriban mwezi mmoja baada ya waasi wanaoshukiwa kuwa wa kundi la ADF kuvamia shule ya Lhubirihakatika eneo la Mpondwe , wilayani Kasesena kuwaua takriban watu 43 , 37 kati yao wakiwa wanafunzi .

Shambulio hilo limesababisha wasiwasi katika taifa hilo na kuzua hofu la ongezeko la mashambulizi ya ADF ambapo vitengo vya usalama katika magharaibi mwa Uganda vimeanza kusitisha burudaniu za usiku.

Chanzo: Bbc