Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni aibuka tena! Atoa neno mapenzi jinsia moja

MUSEVENI WEB Museveni aibuka tena! Aukataa ushoga wazi wazi

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, nchi yake haitaunga mkono vitendo vichafu vya mapenzi ya watu wa jinsia moja.

Rais Museveni amesisitiza kuwa, Uganda haitakumbatia ushoga na kwamba, nchi za Magharibi zinapaswa kuacha kutwisha maoni yao na kulazimisha nchi zinazopingana "kurekebisha" kile alichokiita mkengeuko na uchafu wa kimaadili.

Rais wa Uganda ameongeza kuwa, "tumekuwa tukiwaambia 'tafadhali, tatizo hili la ushoga sio jambo ambalo mnapaswa kuzingatia na kusherehekea,".

Rais Museveni ameeleza kusikitishwa na tabia ya madola ya Magharibi ya kutoheshimu maoni na mitazanmo ya watu wengine na badala yake kung'ang'ania misimamo yao tu na kulazimisha mambo.

Rais Museveni ameyataka mataifa hayo kutambua kwamba, nchi ya Uganda katu haiwezi kuunga mkono vitendo vichafu vya ubaradhuli na ndoa za watu wa jinsia moja.

Mwezi uliopita wa Januari, Rais Yoweri Museveni, aliwaonya watu, wanaharakati na makundi ya wanaotetea ushoga nchini Uganda, akisema ni ujinga kuona baadhi ya watu wanasimamia tamaduni ambazo hazikuwa zao.

Nchi ya Uganda ni moja ya mataifa ambayo yana sheria inayopiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na Rais wa nchi hiyo amekuwa mstari wa mbele kupiga vita vitendo hivyo akisisitiza kwamba, ni kinyume na maadili, vinakinzana na utamaduni wa Kiafrika na ni kinyume na maumbile ya mwanadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live