Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni: Ni ushindi wa tatu

B823ca2020c3615a5066c5000863a316 Museveni: Ni ushindi wa tatu

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amesema Tanzania na Uganda zimepata ushindi wa tatu kwa kusaini makubaliano ya kujengwa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini humo hadi Tanga.

Rais Museveni alisema jana kuwa alikubali bomba la mafuta lijengwe kutika Uganda hadi Tanga kutokana na uhusiano wa kihistoria wa nchi hizo na mchango wa Tanzania katika kuikomboa Uganda.

Aliyasema hayo Ikulu ya Entebbe, Uganda wakati wa hafla ya kusaini mikataba inayoashiria kuanza kwa hatua ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga Tanzania.

Alisema awali, walipata ushindi wa kijeshi, baadaye wa kisiasa, na sasa ushindi wa kiuchumi. Rais Museveni alisema tarehe kama ya jana (Aprili 11) miaka 42 iliyopita majeshi ya Tanzania yaliiteka Kampala na kuiangusha serikali ya Idd Amin. Alisema mwaka 1978/1979 kwa uongozi wa Baba wa Taifa Julius Nyerere, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilifanya kazi kubwa kumuondoa Idd Amin madarakani na mwaka 1985/1986 Nyerere aliwapa silaha.

“Kenya pia ni nchi rafiki kama Tanzania, lakini kihistoria kuna huu mchango wa kipekee wa Tanzania,” alisema Rais Museveni na kubainisha kuwa, mradi huo hauwezi kulipa fidia ya mchango wa Tanzania katika kumpiga Idd Amin na ukombozi eneo la Kusini mwa Afrika ikiwemo Zimbabwe, Angola, Msumbiji, Namibia na Afrika Kusini.

Alisema bomba hilo lenye uwezo wa kubeba mapipa 230,000 ya mafuta kwa siku pia litakuwa chachu ya maendeleo makubwa kwa nchi za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan Kusini wakiamua kulitumia.

Rais Museveni alisema manufaa yatakayopatikana si tu kwa Uganda na Tanzania, bali pia Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kujihakikishia upatikanaji wa mafuta ya uhakika na kwa gharama nafuu.

“Mara ya kwanza sikulipenda wazo la kujenga bomba la mafuta nikijiuliza kwanini tuuze mafuta. Nilijua kuwa kuna watu wanahitaji gei sasa kwanini tujenge bomba…. Niliposikia tutajenga bomba kwenda Tanzania kupitia Tanga, niliunga mkono haraka kwa sababu ya ushirikiano wetu wa kihistoria,” alisema.

Alisema kwenye njia hiyohiyo ya bomba linaweza kujengwa bomba la gesi ili kusafirisha gesi kutoka Msumbiji na Tanzania kuipeleka Uganda na nchi za Maziwa Makuu.

“Tukio hili la leo ni ushindi wa mara tatu kwa Tanzania na Uganda. Namba moja na ushindi wa kijeshi, namba mbili kisisasa na namba tatu sasa kiuchu

Chanzo: www.habarileo.co.tz