Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museven atabiriwa ushindi uchaguzi mkuu

B84ffd22ee51039ff1a08094f75c2469 Museven atabiriwa ushindi uchaguzi mkuu

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA urais kupitia chama tawala cha NRM ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametabiriwa ushindi kubwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na rekodi yake ya kujenga nchi hiyo na kuifanya kuwa ya amani na utulivu.

Wachambuzi wengi wa siasa wanampa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo kiongozi huyo mkongwe barani Afrika dhidi ya Mbunge wa Kyandondo, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kutokana na kile wanachoeleza kuwa ni uchanga katika siasa.

Uganda inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge utakaofanyika Januari 14 mwakani.

Kuna wagombea 11 wanaowania urais, ambapo Rais Yoweri Museveni anatetea kiti chake.

Kwa mujibu wa Katiba ya Uganda, hakuna kizuizi cha mihula wala umri wa juu zaidi kwa wagombea wa urais, hata hivyo umri wa chini ni miaka 18.

Pamoja na Rais Museveni kutabiriwa ushindi, hiyo haiondoi ukweli kuwa atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Bobi Wine pamoja na aliyekuwa kamanda wa jeshi la nchi hiyo, Jenerali Mugisha Muntu, aliyekuwa waziri wa usalama Luteni Jenerali, Henry Tumukunde, Nobert Mao, John Katumba, Patrick Amuriat Oboi, Joseph Kabuleta, Fred Mwesigye na aliyekuwa mwandishi wa habari Nancy Kalembe ambaye ni mwanamke pekee katika kinyanganyiro hicho.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wapigakura 17,658,527 wameandikishwa kushiriki uchaguzi huo na vituo 34,344 vya kupigia kura vimeandaliwa nchini kote.

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini Uganda, mshindi wa kura za urais anatakiwa kupata asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa pamoja na kura moja zaidi.

Chanzo: habarileo.co.tz