Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museven akutwa tena na Virusi vya Corona

Yoweri Kaguta Museven Museven akutwa tena na Virusi vya Corona

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda Yoweri Museveni siku ya jana Jumatano ametangaza kuwa amepima na amekutwa tena na virusi vya Covid-19.

Museveni mwenye umri wa miaka 78 alitengwa baada ya kupimwa na kukutwa na Covid Juni 7, na alipangwa kufanyiwa vipimo vya mwisho siku ya Alhamisi.

Katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye Twitter, Museveni alisema matokeo yake yalikuwa chanya ingawa hakuwa mgonjwa.

"Sijisikii mgonjwa na nilihisi homa kidogo tu katika siku 3 za kwanza. Vinginevyo, ninahisi kuwa tayari kuondoka kwenye hali hii ya kujitenga. Hata hivyo leo tena tulifanya vipimo vya corona na bado nilikuwa na virusi, "alisema Museveni

Kwa hivyo, Museveni alisema atafuta safari ya kidiplomasia siku ya Alhamisi inayowaleta pamoja wakuu wengine sita wa nchi kujadili vita vya Urusi na Ukraine.

“Nilipaswa kujiunga nao kesho. Sasa nimetuma ujumbe rasmi kwamba, kwasababu ya kuendelea kwa hali yangu ya corona, siwezi kujiunga nao. Dr Rugunda atatuwakilisha. Tayari yuko Poland. Kutoka Poland, wataenda Urusi kukutana na Warusi.

Hata hivyo alisema ataweza kuhutubia Bunge la siku ya Alhamisi wakati wa kusomwa kwa bajeti. (Bunge la bajeti)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live