Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume mbaroni kwa mauaji ya mwanaye miaka mitatu

Pingu Law Mume mbaroni kwa mauaji ya mwanaye miaka mitatu

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: Radio Jambo

Polisi Roret, kaunti ndogo ya Bureti wanamshikilia mume na mkewe baada ya mwanamume huyo kudaiwa kumpiga mtoto wake wa miaka 3 hadi kufa.

Kulingana na wanakijiji, mwanamume huyo alidaiwa kumvamia bintiye Jumatano jioni na kumjeruhi vibaya.

Kwa mujibu wa Citizen Digital Wanakijiji hao walifichua kuwa mwanamume huyo huwa anampiga mtoto huyo kila anapofika nyumbani kutoka kwenye ulevi wake kwa madai kuwa si babake mzazi.

Majirani walisema siku hiyo ya maafa, mwanamume huyo alifika nyumbani na kuibua ugomvi na mkewe kabla ya kumgeukia binti huyo kwa makofi na mateke hadi kupoteza fahamu.

Walifichua kuwa kila mwanamume huyo alipokuwa akinywa pombe, marafiki zake kwa kawaida walimdhihaki kwa madai ya kuoa mwanamke mwenye mtoto, jambo ambalo lilimkasirisha mwanamume huyo.

Alipokuwa akimshambulia mtoto huyo, mama huyo alitoa tahadhari ambayo ilivuta hisia za wanakijiji wengine ambao walikimbilia eneo la tukio na kumkimbiza mtoto huyo katika Kituo cha Afya cha Roret ambapo huduma ya kwanza ilitolewa kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kericho kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, mtoto huyo alifariki kutokana na majeraha hayo wakati madaktari walipokuwa wakijaribu kumfufua.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kericho waliarifiwa kuhusu kisa hicho na kuwakamata wawili hao hospitalini.

Mwili wa mtoto huyo ulihamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo hiyo.

Chanzo: Radio Jambo