Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume aliepakaziwa na Mkewe na mwanae kesi ya ubakaji asamehe (+picha)

Screenshot 2020 12 18 At 10.25.19 660x400.png Mume aliepakaziwa na Mkewe na mwanae kesi ya ubakaji asamehe (+picha)

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Mkenya Julius Wambua Musyoki ametoka rasmi Gerezani baada ya kutumikia kifungo kwa miaka 8 kwa kosa la kumbaka Mtoto wake wa miaka 15, uamuzi ambao umebatilishwa na Mahakama baada ya kujiridhisha kuwa Julius hakubaka bali alipakaziwa na Mtoto wake na Mkewe.

Jaji George Odunga amesema Mtoto huyo aitwaye Dorcas alikula njama na Mama yake na akafundishwa kuidanganya Mahakama kwasababu Mwanamke huyo alikuwa na mgororo na Mumewe, Julius alihukumiwa kifungo cha Maisha.

Moja ya mambo yaliyogusa hisia za Watu ni kitendo cha Julius kutangaza kuwa amewasamehe Mwanae Dorcas na Mkewe licha ya kumfanya akae Jela kwa miaka 8, nje ya Gereza la Kamiti Julius ameikumbatia Familia yake na kusema>> “Mke wangu pia atafute muda aniombe msamaha ila Mimi nimewasamehe” .

SIMANZI: MAELFU YA WATU WALIVYOUPOKEA MWILI WA BILIONEA SUBASH PATEL KIWANDANI KWAKE

Chanzo: millardayo.com