Mwanamume mwenye umri wa miaka 56 anakabiliwa na wakati mgumu kuwalewa watoto saba, baada ya mkewe kumuacha na kuamua kuishi na kakake mdogo.
Simon Murefu Muyeho alisema kuwa kaka yake mdogo, ambaye ni mhudumu wa bodaboda alikua akimpa lifti mkewe Farida, ndipo wakazoeana, kupendana na kuamua kuishi pamoja.
"Nilifuatilia suala hili na kumuambia kaka yangu anarejeshee mke wangu ila akakataa. Hata hivyo sijakata tamaa. Jambo hili likiendela nitamshtaki kwa mamlka husika ili kutatua shida hii," Muyeho aliiambia Afrimax English.
Muyeho alisema kwamba kakake alikuwa akikana kwamba amempokonya mke, licha ya uvumi kusambaa kwamba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Farida, ambaye alikuwa mfanyabiashara alisema mumewe Muyeho alikuwa akimtesa.
"Alikuwa akinipiga kila wakati akitoka kazini. Alikuwa ni bawabu na kila asubuhi alikuwa akija nyumbani akiwa mlevi. Nusra aniue ila nilinusurika. Pia alianza kuwa na mipando ya kando.
"Kuna siku alinichoma na kunivunja mkono. Ndipo unaniona nimelemaa. Kuna wakati tulilala njaa nispojitahidi tupate chakula. Hakuwajibika," mama huyo wa watoto saba alisema.
Mama apigwa marufuku kuwaona wanawe
Farida aliongeza kusema kwamba mumewe amekataa asiwaone wanawe baada ya kuanza kuishi na kaka yeke mdogo.
Farida amekiri kumpenda sana kaka ya mumewe kwa sababu anajua kumtunza na hukidhi mahitaji yake ya kila siku.
Mume mpya wa Farida anasema kwamba shemeji yake hakuwa akiishi kwa amani na kaka yake, ndipo akapata fursa ya kuwa naye.