Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume aandaliwa sherehe maridadi ya Birthdei na wake zake watano

E9d9730e37f9df9a Mume aandaliwa sherehe maridadi ya Birthdei na wake zake watano

Mon, 5 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Wanawake watano kutoka Uganda waliandaa sherehe kubwa ya siku ya kuzaliwa kwa mume wao

- Hajji Ngobi, anaripotiwa kuwa mwanabiashara mashuhuri ambaye anapendwa sana na wake zake kwa kuleta amani kati yao

- Mwanamume huyo mwenye miaka 57, alisifiwa sana na hata kudodonkwa machozi wake zake walipokuwa wakitoa hotuba zao

Wanawake watano ambao wameolewa na mwanamume mmoja wameonyesha mapenzi yao ya dhati kwake katika njia ya kipekee.

Wanawake watano kutoka mjini Iganga, Uganda waliandaa sherehe kubwa ya siku ya kuzaliwa kwa mume wao Hajji Ngobi akitimia miaka 57.

Kulingana na Nile Post, sherehe hiyo iliandaliwa katika moja ya boma la wake hao kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mume wao ambaye amekuwa pamoja nao kati ya miaka 10 hadi 30 kwenye ndoa.

Watano hao ni Aisha Namatende, Sharifah Ngobi, Aminah Namukose, Zalufah Nampina na Hajjati Lamulal Ngobi.

Ngobi, anaripotiwa kuwa mwanabiashara mashuhuri na pia waziri mkuu wa kabila la Nagwere.

Wake hao pia walimumiminia mume wao na zawadi kochokocho katika hafla ambayo marafiki na familia walihudhuria.

Wanawake hao walimshukuru Hajji kwa kuhakikisha kuna amani kati yao na kuwagawanyia mali bila upendeleo.

Mwanamume huyo mwenye miaka 57, alisifiwa sana na hata kudodonkwa machozi wake zake walipokuwa wakitoa hotuba zao.

Hajji aliwashukuru wake zake akisema kuwa hakutarajia kwamba angeliandaliwa karamu huku akitoa ushauri kwa wale ambao wangependa kuoa zaidi ya mke mmoja.

“Nimeweza kuwajengea wake zangu wote nyumba na wote wana biashara. Kabla ya kuongeza mwingine, mimi huwa wazi kwake na kumuambia hayuko pekee yake," alisema.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke