Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muimbaji Bahati apakia video akivuta sigara na kuwachanganya wafuasi wake

3fb389564db326a0 Muimbaji Bahati apakia video akivuta sigara na kuwachanganya wafuasi wake

Tue, 8 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Bahati aliwashtua wafuasi wake baada ya kupakia video yake akivuta sigara

- Msanii huyo ambaye alikuwa anavuma na nyimbo za injili, alionyesha weledi wake wa kuvuta sigara

- Video hiyo iliibua hisia mseto miongoni mwa wafuasi wake huku wengi wakikumbuka maisha yake ya awali akiwa mwanamuziki wa injili

Bahati ameibua mjadala moto kwenye mtandao wa kijamii baada ya kupakia video yake akivuta sigara.

Video hiyo iliyopakiwa Juni 7, 2021, inamuonyesha Bahati akiwa amevalia suti na miwani ya jua akivuta sigara huku mwanamke akiwa amesimama kando yake.

Kutokana na namna alikuwa anapiga mapafu, ni dhahiri kwamba ana weledi wa kuvuta sigara.

Katika jumbe, Bahati alifichua kuwa video ni kutoka kwa kibao chake ambacho atawachia Juni 8.

Kulingana na mwanamuziki huyo, wimbo huo utakuwa wake wa kwanza kuachia kutoka kwa albamu yake ya Just In Love.

Video hiyo iliibua hisia mseto miongoni mwa wafuasi wake huku wengi wakikumbuka maisha yake ya awali akiwa mwanamuziki wa injili.



Hii hapa baadhi ya maoni:

@alex_mwakideu: "Kutoka kwa mtoto wa mama hadi mtoto wa jambazi. Kila heri'

@ringtoneapoko: "Kutoka kuwa muimbaji wa injili hadi muathiriwa wa dawa za kulevya. Hata hivyo, mimi ndio nadhibiti muziki wa injili."

@mcatricky: "Vuta kabisa. Unaweza hata kuenda mubashara Moshi (Tanzania)."

@krgthedon "Baba Heaven jamani?"

@honalinur: "Hii ni nini kaka yangu?"

@iam_monchy: "Tumempoteza kabisa muimbaji wa injili."

Katika mahojiano ya awali na MC Jessy, muimbaji huyo alisema huenda atagura kuimba nyimbo za injili.

"Siwezi kumuwacha Kristu. Hii ndio muhimu sana kuliko nyanja ya injili ambayo imeoza," alisema.

Huenda posti ya Bahati ni biashara hatua ambayo inalenga kumchumia mapato mengi kutoka kwa tasnia ya muziki wa kidunia.

Sadfa ni kuwa wiki moja iliyopita muimbaji wa nyimbo zainjili Guardian Angel alipuzilia mbali madai kuwa nyimbo za injili hazilipi.

“Endapo upo katika tasnia ya injili kwa sababu ya pesa, ungelikuwa umeondoka kitambo kwa sababu hakuna pesa. Ni dhana potovu tu.Ukichukulia injili kama huduma basi Mungu atakubariki," alisema.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke