Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhoozi apandishwa cheo kuwa Jenerali

Muhoozi Museveni.png Muhoozi apandishwa cheo kuwa Jenerali

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda amempandisha cheo Mtoto wake Muhoozi Kainerugaba kuwa Jenerali ikiwa ni cheo kikubwa zaidi cha kijeshi Uganda ambapo kabla ya hapo alikua na cheo cha Luteni Jenerali.

Museveni amempandisha cheo Muhoozi lakini hata hivyo amemuondoa kwenye nafasi ya Ukamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda na nafasi yake inachukuliwa na Meja Jenerali Kayanja Muhanga ambaye kwa sasa ni Kamanda wa Operesheni Shujaa inayoendeshwa nchini DRC.

Muhoozi ambaye amezua mijadala Twitter tangu jana baada ya kutangaza kutaka kuiteka Nairobi na kusema anataka Afrika Mashariki ziungane na kuwa Taifa moja mapema leo alisema huenda Baba yake akafanya mabadiliko kwenye Jeshi.

Muhoozi aliandika “Nilikuwa na mazungumzo na Baba asubuhi leo, Tweets zangu zimewatishia sana Wakenya, Baba atatangaza mabadiliko, kuna maombi maalum nayafanya kwa ajili ya Jeshi letu”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live