Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemuondoa Mtoto wake Muhoozi Kainerugaba kwenye nafasi ya Ukamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda na nafasi yake inachukuliwa na Meja Jenerali Kayanja Muhanga ambaye alikuwa Kamanda wa Opereshemi Shujaa inayoendeshwa nchini DRC, Kayanja amepandishwa pia cheo na kuwa Luteni Jenerali.
Muhoozi ambaye amezua mijadala kwenye mtandao wa Twitter tangu jana baada ya kutangaza kutaka kuiteka Nairobi na kusema anataka Nchi za Afrika Mashariki ziungane na kuwa Taifa moja mapema leo alisema huenda Baba yake akafanya mabadiliko kwenye Jeshi.
Muhoozi aliandika “Nilikuwa na mazungumzo na Baba asubuhi leo, Tweets zangu zimewatishia sana Wakenya, Baba atatangaza mabadiliko, kuna maombi maalum nayafanya kwa ajili ya Jeshi letu”