Mshauri mkuu wa rais wa operesheni maalumu, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amewafariji walinda amani wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) wanaohudumu chini ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kutokana na tukio hilo la kusikitisha katika kituo chao cha Buulo Mareer mnamo Mei 26, 2023. Daily Monitor limeripoti.
Rais Museveni siku ya Jumamosi alisema Uganda ilipoteza wanajeshi 54, rekodi mbaya zaidi ya Jeshi hilo wakiwa Somalia.
Alikitahadharisha kikosi kutojibweteka badala yake kuwa na ujasiri.
Jenerali Muhoozi amekuwa Somalia kwa siku tano zilizopita akikutana na makamanda na wafanyakazi wa UPDF, pamoja na manusura wa tukio la Buulo Mareer.