Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mugabe angekuwa hai leo angetimiza miaka 100

Mugabe 1280322 Mugabe angekuwa hai leo angetimiza miaka 100

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anaitwa Robert Gabriel Mugabe ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Afrika waliokuwa na misimamo mikali kwa ajili ya kulinda heshima na utu wa Waafrika.

Alikuwa Waziri mkuu wa Zimbabwe mwaka 1980 mpaka 1987, alikuwa Rais wa Zimbabwe kuanzia mwaka 1987 mpaka 2017, ni miongoni mwa Ma-rais waliodumu kwa muda mrefu madarakani barani Afrika.

Alikuwa kiongozi wa chama cha "Zimbabwe African National Union (ZANU)" kuanzia mwaka 1975 mpaka 1980 baada ya chama hicho kubadilika kuwa "ZANU – Patriotic Front (ZANU–PF)" pia alikuwa kiongozi kuanzia mwaka 1980 mpaka 2017.

Mugabe ni miongoni mwa viongozi barani Afrika waliokuwa na ukaribu mkubwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mara kadhaa mbele ya watu alikuwa akisifu mchango wa Nyerere katika kujenga na kukuza umoja, amani na mshikamano barani Afrika.

Mugabe alizaliwa 21 Februari 1924, alifariki Septemba 6 2019 akiwa na umri wa miaka 95, hivyo angekuwa hai leo hii angetimiza miaka 100.

R.I.P Robert Gabriel Mugabe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live