Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muda wa walinda amani wa UN nchini Mali umekamilika

Walinda Amani UN Wasimamishwa Madai Ya Unyanyasaji Wa Kingono DR Congo Muda wa walinda amani wa UN nchini Mali umekamilika

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa walinda amani wa Umoja wa mataifa nchini Mali umemaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 10, msemaji wa UN amethibitisha.

Hatua hii imekuja baada utawala wa kijeshi nchini humo kutaka Umoja wa Mataifa kuwaondoa walinda amani wake.

Ujumbe huo ambao unafahamika kama MINUSMA, umeshusha bendera za Umoja wa Mataifa katika makao makuu yake jijini Bamako, msemaji wake Fatoumata Kaba ameeleza.

Jour solonnelle. C’est la cérémonie de fin de mission de la MINUSMA aujourd’hui.

A solemn day. It's MINUSMA's end-of-mission ceremony today. pic.twitter.com/RtWdk43KSW — Fatoumata Sinkoun Kaba (@FatiKaba) December 11, 2023

Kwa mujibu wa Fatoumata Kaba, tukio hilo linaashiria kumalizika rasimi kwa muda wa ujumbe huo japokuwa baadhi ya maofisa wake wangali kwenye taifa hilo.

Utawala wa kijeshi nchini Mali ambayo ulichukua madaraka mwaka wa 2020, mwezi Juni ulitoa wito kwa UN kuwaondoa wanajeshi wake katika ardhi yake ambao walitumwa huko mwaka wa 2020. Wanajeshi wa UN wamekuwa wakikabiliana na makundi ya watu wenye silaha nchini Mali Wanajeshi wa UN wamekuwa wakikabiliana na makundi ya watu wenye silaha nchini Mali © Moulaye Sayah/AP

Hatua ya kuondoka kwa wanajeshi hao inakuja licha ya nchi hiyo ya Sahel kuendelea kukabiliwa na tishio la makundi yenye silaha.

Kumekuwepo na hofu kuwa kuondoka kwa wanajeshi wa UN, kutasababisha kuongeza kwa makabiliano ya kudhibiti baadhi ya maeneo kati ya wanajeshi na makundi ya watu wenye silaha. Tangu mwaka wa 2012, Mali imekuwa ikikumbwa na vitendo vya makundi yenye mafungamano na Al-Qaeda na Islamic State, ghasia zinazofanywa na makundi yaliyotangaza kujilinda na ujambazi. Tangu mwaka wa 2012, Mali imekuwa ikikumbwa na vitendo vya makundi yenye mafungamano na Al-Qaeda na Islamic State, ghasia zinazofanywa na makundi yaliyotangaza kujilinda na ujambazi. © AFP

MINUSMA ilikuwa na maofisa wa usalama karibia 15,000 nchini Mali ambapo karibia 180 wameuwa katika wakiwa kazini katika mazingira hatari.

Tangu watakiwe kuondoka, walinda usalama wa MINUSMA wameondoka katika maeneo 13 nchini Mali na wanatarajiwa kufunga kambi zao katika mji wa Gao na Timbuktu kaskazini mwa taifa hilo.

Juma lililopita, Ujumbe huo wa UN ulipeana kambi ya Mopti katikati mwa Mali kwa mamlaka mojawapo ya maeneo ambayo yanakabiliwa na utovu wa usalama kutoka kwa wanajihadi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live