Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muda wa kufanya kazi benki wapunguzwa

Central Bank Rwanda Ktpress Muda wa kufanya kazi benki wapunguzwa

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KWA mujibu wa masharti mapya ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona yaliyotolewa na wizara ya afya, benki karibu zote nchini Rwanda zimepunguza muda wa kufanya kazi ili kuwaruhusu watumishi wake kutekeleza masharti hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Mabenki Rwanda (RBA), benki zote zitakuwa zikifungwa saa 10:00 jioni isipokuwa katika wilaya ya Musanze ambako zitafungwa kuanzia saa 9:00 alasiri.

Taarifa hiyo ilisema utaratibu huo utaanza rasmi leo, lengo likiwa ni kuwapa nafasi ya kutosha watumishi wa benki waweze kufika majumbani kwao kabla ya muda wa mwisho uliowekwa na serikali kwa kila mwananchi awe nyumbani kwake.

Wizara ya Afya mwishoni mwa wiki ilitoa utaratibu mpya wa namna ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona ambapo mwisho wa wananchi kuwa nje itakuwa kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 10:00 alfajiri.

Hatua hizo kali zitaanza kutumika leo hadi Januai 4 mwakani.

Kwa upande wa wilaya ya Musanze, mwisho wa kutoka nje ni kuanzia saa 1:00 usiku hadi saa 10:00 alfajiri.

Wizara ya Afya imelitaja eneo la Musanze kuwa lililoathiriwa zaidi na virusi vya corona kwa muda mrefu hivyo kuzidisha vizuizi katika eneo hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz