Dar es Salaam. Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 38, nchini Afrika Kusini amebainika kuwa na virusi vya corona. Afrika Kusini imeripoti kesi hiyo kuwa ya kwanza nchini humo, huku idadi ya watu walioripotiwa kukutwa na virusi vya ugonjwa huo barani Afrika hadi sasa kufikia 27. Algeria ndio nchi ambayo iliathiriwa vibaya na ugonjwa wa corona ambapo kesi 17 za ugonjwa huo ziliripotiwa kutokea nchini humo, ikifuatiwa na Senegal iliyoripotiwa kuwa na kesi 4 za watu wenye virusi vya ugonjwa huo. Waziri wa Afya Afrika Kusini, Zweli Mkhize amesema kuwa mtu huyo pamoja na mkewe wenye watoto wawili, ni miongoni mwa kundi la watu 10 waliorejea nchini humo wakitokea Italia, Machi 1, mwaka 2020. Taarifa kutoka Afrika Kusini zilieleza kuwa madaktari waliohusika katika kumhudumia mtu huyo aliyebainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona, walifanya huduma hiyo katika eneo maalum lililotengwa kwa kazi hiyo. Timu ya wataalamu imetumwa katika eneo la mashariki mwa jimbo la KwaZulu-Natal, ili kuwabaini watu wanaodhaniwa kuwa huenda walihusiana au kugusana na mtu huyo ayekutwa na virusi hivyo, alisema Waziri wa Afya Afrika Kusini, Zweli Mkhize. Wakati huohuo watu wengine wawili raia wa Afrika Kusini ambao walilazwa hospitali nchini Japan baada ya kubainika kuwa na virusi vya corona, wameripotiwa kupona na wanaweza kurudi nyumbani hivi karibuni, maofisa wameeleza.