Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa miaka 4 alawitiwa na mpenzi wa mama yake

Wnanaume Saba Rape Mtoto wa miaka 4 alawitiwa na mpenzi wa mama yake

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa kiume miaka minne anaendelea kupata nafuu katika hospitali moja ya Nairobi baada ya mpenzi wa mamake, mwendesha bodaboda, kudaiwa kumlawiti mara kadhaa.

Mtoto huyo mdogo, mwanafunzi wa PP1, anasemekana kulawitiwa na mshukiwa mwenye umri wa miaka 32 mara nyingi wakati mama yake akiwa hayupo.

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilisema kwamba mtoto huyo aliamua kumweleza mwalimu wake kuhusu unyama huo aliofanyiwa, ambapo mwalimu naye aliripoti kwa polisi.

"Mtoto huyo alisimulia mwalimu wake jinsi mpenzi wa mamake ambaye ni dereva bodaboda, alivyokuwa akimpiga na kumfanyia unyama huo wakati mama yake akiwa hayupo," DCI alisema.

Idara ya uchunguzi ilifichua zaidi kwamba mwalimu huyo aliwasilisha ripoti ya polisi baada ya kugundua kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na maumivu makali akiwa shuleni.

Maafisa wa upelelezi waliokuwa katika Kituo cha Polisi cha Parklands kisha wakamsaka haraka na kumkamata mama yake mtoto huyo pamoja na mpenzi wake.

Wawili hao wanazuiliwa chini ya ulinzi halali wakisubiri kufikishwa mahakamani huku uchunguzi wa kesi hiyo ukiendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live