Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa hayati Gaddafi atangaza kugombea Urais Libya

AFP Saif Al Islam Gaddafi Presidential Candidate Registration 0 Mtoto wa hayati Gaddafi atangaza kugombea Urais Libya

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: BBC

Mtoto wa kiume wa aliyekua Rais wa Libya Muammar al-Gaddafi amejisajili kama mgombea wa kwanza wa Urais wa moja kwa moja katika uchaguzi wa urais wa mezi ujao.

Saif al-Islam Gaddafi wakati mmoja alitarajiwa kuwa mrithi wa baba yake, lakini hatua yake ya kuunga mkono msakao wa kikatili dhidi ya waandamanaji mika 10 iliyopita ilimchafulia sifa.

Tangu kuibuka kwa maandamano ya mwaka 2011 ya kupinga serikali, Libya imekumbwa na mzozo.

Makundi ya kutetea haki yameelezea wasiwasi wao kuhusu uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Disemba 24, ikiwa utakuwa huru na wa haki.

Nchi zenye uwezo mkubwa duniani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wameonya kuwa mtu yeyote atakayejaribu kuvuruga au kufanya udanganyifu atakabiliwa na vikwazo.

Picha na video zinazosambazwa mitandaoni zinamuonesha Saif al-Islam Gaddafi akiwa kwenye bango la uchaguzi, akisaini makaratasi ya uchaguzi.

Chanzo: BBC