Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Ruto akanusha madai ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Ruto Nick Nickson William, Kushoto akiwa na baba yake William Ruto

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa Ruto, Nickson William, ameweka bayana kuhusu madai ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja mara baada ya kusambaa kwa video yenye utata iliyochukuliwa katika sherehe yake ya siku ya kuzaliwa.

Kipande hicho cha video kilichosambaa katika mitandao ya kijamii kilimuonesha mwanaume mwenye asili ya kihindi akiwa ana mvalisha cheni kijana huyo huku watu waliokuwepo eneo hilo wakishangilia kwa furaha.

Kitendo hicho kimeibua minongono mingi katika mitandao ya kijamii huku wengi wakimshtumu kwa kuhusika na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja maarufu kama ushoga.

Hata hivyo Nick amekanusha madai hayo kwa kusema kuwa hausiki na vitendo hivyo, isipokuwa kilichokuwa kinaendelea siku hiyo ni utoaji tu wa zawadi, na kuwa alipokea zawadi hiyo kutoka kwa swahiba wake huyo mkubwa.

Aidha amewataka watu wajitahidi kutengeneza marafiki ambao watawafurahia kila wanapopanda kimaisha, ikiwa ni pamoja na kupeana zawadi katika siku muhimu kwenye maisha yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live