Mtoto wa Rais wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni kwa mara nyingine tena amezua tetesi kuwa yuko katika mstari wa kumrithi baba yake.
Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba "atalipa fadhila kwa nchi yake" kwa kuwa rais.
Mnamo Mei mwaka huu, mwanajeshi huyo aliuliza kwenye Twitter ikiwa watu walidhani anafaa kugombea urais na mapema mwezi huu aliandika:
"Kwa upinzani wa Uganda, baada ya baba yangu, nitawashinda vibaya katika uchaguzi wowote, Waganda wananipenda zaidi kuliko nyinyi''
Jenerali huyo mwenye umri wa miaka 48 si mgeni kwenye mabishano kwenye Twitter.
Mwanzoni mwa Oktoba, alitishia katika ujumbe wake wa Twitter kuivamia nchi jirani ya Kenya, na hivyo kusababisha kuomba radhi kwa umma na mikutano ya kidiplomasia ili kuthibitisha uhusiano huo.
Kisha baadae Rais Museveni kuagiza kwamba akome kutoa maoni yake kuhusu masuala ya serikali kwenye Twitter, Jenerali Kainerugaba alisema kwamba "hakuna mtu atakayempiga marufuku kwa chochote".