Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Museveni aanika mpango wake kuiteka Kenya

Mtoto Wa Rais Museveni Mtoto wa Museveni aanika mpango wake kuiteka Kenya

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa rais Yoweri Museveni wa Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ameandika kwenye mtandao wake wa twitter kuhusu kutofurahishwa kwakwe na hatua ya Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta, katika uchaguzi wa hivi karibuni, kutogombea kwa muhula wa tatu wa urais, kinyume na katiba ya Kenya.



Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba pia aliandika katika mtandao huo kwamba hapendezwi na katiba au utawala wa sheria. "Kwetu sisi ni mapinduzi tu na hivi karibuni mtajifunza kuhusu hilo," alisema kwa kwa mafumbo.



Wapo wanaoeleza kwamba Luteni Jenerali Kainerugaba, ambaye anajulikana kwa 'kauli tata' mitandaoni, anaandaliwa kuchukua nafasi ya baba yake, Museveni, kama ajaye rais wa Uganda.

Rais Museveni amekuwa madarakani tangu 1986. Na tangu wakati huo, Kenya imeshabadilisha marais mara tatu. Baadhi ya Wakenya walibaki kushangazwa na Kainerugaba alikiandika, wakihoji kama yuko sawa.

Lakini Mtoto huyo wa Museveni alisema jeshi lake linaweza kuuteka mji mkuu wa Kenya, Nairobi katika muda wa wiki mbili.



Huku akionekana kufurahia majibizano kwenye mtandao huo wa Twitter kuna wakati aliuliza: "Je baada ya jeshi letu kuteka Nairobi, niishi wapi? Westlands? Riverside?"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live