Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Museveni: Nakuja Tanzania

Muhoozi Kainerugaba Samia Suluhu Hassan Mtoto wa Museveni: Nakuja Tanzania

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa zamani wa Jeshi la Ardhini la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema anajiandaa kuja Tanzania nchi ambayo amezaliwa na kwamba atakuwa na furaha kuitembelea Tanzania na kumpa salamu za heshima Rais Samia Suluhu.

Muhoozi amesema safari yake inayofuata ataitembelea Tanzania na kwamba atafurahia kufika kwenye ardhi aliyozaliwa na kumpa salamu zangu zake za heshima Rais Samia ambaye amemuita Kiongozi Mkuu Mwanamke Afrika.

Muhoozi ameipost pia picha ya Rais Samia kwenye akaunti yake ya Twitter na kuandika; “Rais wa Waswahili kama Mimi, Mtukufu Samia Suluhu Hassan, Mungu ambariki.”

Muhoozi alizaliwa April 24,1974 Dar es salaam Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live