Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Museven amjibu baba yake 'hakuna wa kunizuia mitandaoni'

Mambo 10 Kumhusu Mtoto Wa Rais Museveni Mtoto wa Museven amjibu baba yake 'hakuna wa kunizuia mitandaoni'

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kusema kuwa mtoto wake, Muhoozi Kainerugaba atakaa kando kwenye mtandao wa Twitter linapokuja suala la mijadala ya mambo ya Serikali, mwenyewe amesema hakuna wa kumzuia.

Jumapili iliyopita katika mahojiano yaliyorushwa na KTN ya Kenya, Rais Museveni alisema, "Ataondoka Twitter. Twitter sio tatizo, tatizo ni kile unachoandika. Kuzungumza kuhusu nchi nyingine na siasa za upendeleo za Uganda ni jambo ambalo hapaswi kufanya na hatalifanya."

Jana Jumanne Oktoba 18, 2022 katika mtandao huo, Jenerali Muhokozi amesema kuwa yeye ni mtu mzima na hakuna wa kumpiga marufuku kwa kitu chochote.

“Namesikia mwanahabari kutoka Kenya akimuuliza babaangu anipige marufuku kwenye kwa Twitter? Je, huo ni utani? Mimi ni mtu mzima na hakuna mtu atakayenipiga marufuku kwa kitu chochote,” ameandika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live