Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto hufa kila baada ya saa mbili Sudan

Mtoto Hufa Kila Baada Ya Saa Mbili Sudan Mtoto hufa kila baada ya saa mbili Sudan

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka MSF linaonya kuwa Sudan inakabiliwa na baa kubwa la njaa ambalo ni kubwa na la kutisha kuliko hata walivyokadiria hapo awali.

Shirika hilo limewafanyia uchunguzi wa kiafya maelfu ya watoto na wanawake walioko katika kambi ya watu walioachwa bila ya makazi katika jimbo la kaskazini la Darfur na kugundua kuwa theluthi moja ya wanaoishi katika kambi hiyo wanakabiliwa na utapia mlo.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan vilivyoanza mwaka mmoja uliopita kati ya jeshi la nchi hiyo na kundi maalum la wanamgambo la RSF limeitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF linasema kila baada ya saa mbili,mtoto mmoja anafariki dunia katika kambi ya Zam Zam.

Jumatatu wiki ijayo 15 Aprili, itakuwa mwaka mmoja kamili tangu mzozo huo wa Sudan kuzuka,mzozo ambao umeacha zaidi ya nusu ya idadi jumla ya watu wake wakihitaji kwa dharura misaada ya kibinadamu.

Mamilioni wameachwa bila ya makazi,wakikabiliwa na hatari ya kufa njaa,kushambuliwa kwa njia mbalimbali,wanawawe na wasichana wakinyanyaswa kingono,watoto wakiacha masomo na miundo mbinu ikiharibiwa vibaya.

Umoja wa Mataifa unasema Sudan inashuhudia mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu na kuwa na idadi kubwa ya watu waliaochwa bila ya makazi duniani huku maafisa wa kutoa misaada nchini humo wakivitaja vita vya Sudan vilivyosahaulika licha ya kuwaaathiri zaidi ya watu milioni ishirini na nne.

Wataalamu wa masuala ya kiusalama wana wasiwasi kuwa ufumbuzi wa mzozo huo kati ya mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah al Burhan na aliyekuwa makamu wake Jenerali Mohamed Hamdan Daglo hauonekani kupatikana hivi karibuni.

Chanzo: Bbc