Katika hali isiyokuwa ya kawaida kichanga cha miezi saba amekutwa ndani ya nyumba akinyonya matiti ya marehemu mama yake aliyefahamika kwa jina Dorcas Chirwa (20).
Tukio hilo limetokea oktoba 17 mwaka huu wilayani Chongwe nchini Zambia baada ya wazazi wa mtoto huyo kudaiwa kuuana na kumuacha mtoto huyo akiwa analia.
Inaelezwa mmoja wa majirani ndiye aliyesikia kelele za kichanga hicho kisha kwenda kuvunja mlango na kukuta akiwa ananyonya matiti ya mwili wa marehemu mama yake uliokuwa umelala sakafuni ukiwa umetapakaa damu.
Kulingana na ripoti ya Naibu Ofisa Uhusiano wa Umma wa Polisi, Danny Mwale, amesema jirani huyo aligundua nyumba hiyo ilikuwa kimya ambavyo siyo kawaida lakini alisikia sauti ya mtoto akiwa analia jambo lililomlazimu kuingia ndani kwa nguvu.
“Alikuta Dorcas amekufa huku mwili wake ukiwa amelala kwenye dimbwi la damu huku mtoto wake mchanga akinyonya titi lake,” ilielezea ripoti.
Vilevile uligunduliwa pia mwili wa mume wa Dorcas ukiwa umenining'inia kwenye dari, kwa kujiua.
Ripoti hiyo inasema vifo hivyo vilitokana na mzozo wa ndoa ambapo mume anadaiwa kutumia stuli kumuua mkewe kisha nayeye kijiua.
Kichanga hicho kimefikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chongwe kwa ajili ya uangalizi, huku polisi wakianzisha uchunguzi kuwatafuta ndugu wa wawili hao.