Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtihani wa KCSE 2020: Wanafunzi zaidi ya 280 kukosa matokeo

De18d08ad4f74e81 Mtihani wa KCSE 2020: Wanafunzi zaidi ya 280 kukosa matokeo

Mon, 10 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wizara ya afya imetangaza rasmi matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne hii leo Jumanne, Mei 10 ambapo mwanafunzi bora alipata gredi ya A.

Mtahiniwa Simiyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka wa kwanza kwa maksi 87.334.

Hata hivyo, Waziri magoha ametangaza kwamba watahiniwa 287 wa mtihani huo hawatapokea matokeo yao kwa ajili ya kujihusisha na udanganyifu wakati wa mtihani.

Magoha alisema wanafunzi hao walinaswa kwa kujaribu kuiba mitihani kwa kutumia simu za rununu au maandishi kwenye sare zao za shule.

Akihutubia taifa akiwa katika jumba la Mtihani House, Waziri Magoha alisema shule zote zitapokea matokeo ya mtihani huo japo huenda kukawa na mabadiliko baada ya kukamilika kwa uchunguzi unaoendelea.

Kulingana na arifa ya Magoha, shule 20 huenda zikakosa kupokea matokeo ya mtihani iwapo zitapatikana na hatia ya wizi wa mitihani.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, watahiniwa 893 walipata gredi ya A huku 143, 140 wakipata alama zitakazowawezesha kuingia moja kwa moja katika Vyuo Vikuu.

Takwimu za Baraza la kitaifa la mitihani nchini, KNEC zinaonyesha kuwa watahiniwa 752,933 walisajiliwa kufanya mtihani wa KCSE mwaka uliopita katika vituo 10,437.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke