Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtengeneza mabomu wa ADF akamatwa Uganda

Bomu Lililotegwa Katika Mkokoteni Wa Punda Laua Afisa Wa Polisi Wa Kenya.jpeg Bomu

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashambulizi ya kila wakati ya kundi la ADF yamekuwa yakisababisha vifo na kuwalazimisha watu kuyakimbia makaazi yako mashariki mwa Kongo.

Kamanda huyo, Anywari Al-Iraq, ambaye ni raia wa Uganda, amekamatwa kwenye misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambako kundi hilo la ADF limekuwa likiendesha operesheni zake.

Taarifa ya jeshi la Uganda imesema kwenye oparesheni iliyofanikisha kukamatwa kwa Al-Iraq huko mkoani Ituri, watu wanane ikiwemo watoto kadhaa wameokolewa. Limesema pia limebaini shehena ya malighafi zinazotumika kutengeneza mabomu ya kienyeji.

Kundi la ADF lenye mafungamano na lile linalojiita Dola la Kiislamu lilianza kama harakati ya uasi nchini Uganda lakini limepiga kambi nchini Kongo tangu mwishoni mwa miaka ya 1990. Linatuhumiwa kufanya mauaji ya mamia ya wanavijiji kwenye uvamizi ambao imekuwa ikifanya miaka ya karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live